KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM
PAROKIA YA MT. YOHANE PAULO II - BUYUNI

Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.

Neno Linalotuongoza

Zab 27:4

Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.

Tumsifu Yesu Kristo!

Wapendwa Taifa la Mungu: Waumini wa Kanisa Katoliki wa eneo la Buyuni walianza kusali kila Jumapili katika darasa moja la shule ya msingi Buyuni kuanzia mwaka 1986 – 1990, ibada au misa iliendeshwa na Padre Minhard. Mwishoni mwa mwaka 1990 Pd. Minhard alijenga kanisa dogo eneo la mgeule juu na waumini wa kikatoliki walikuwa wachache sana takribani 15 – 20. Miaka  ya 1990 – 1996  baada ya Padre Minhard kuhamishwa aliletwa Baba Paroko G. Say, waumini walikuwa bado wachache na majitoleo pia hayakuwa yakutosha. Kati ya mwaka 1996 – 2000 Paroko alikuwa Padre Stephen Nyilawila, kipindi hiki waumimi waliongezeka kiasi na kufikia kati ya 70 – 80. Kufikia mwaka 2001 – 2003 tulikuwa na Padre Lucas Kidegu ni kipindi yalipoanza mafundisho ya dini na hatimaye Ubatizo kwa walioamini kumfuata Yesu Kristo.

Matukio Katika Picha

Huduma za Kiroho

      1. 1. Misa Takatifu tatu kila Jumapili na katikati ya wiki kila asubuhi (Jumatatu, Jumanne, Jtano, Ijumaa).
      1. 2. Misa takatifu kila jumapili kwa Kigango cha Mt. Stephano – Kigezi Misa 2, Kigango cha Mt. Antony wa Padua Nyeburu misa 1 na Kituo cha Sala Mt. Cecilia – Zavala misa 1.
      1. 3. Ibada za Sikukuu zote mkesha na sikukuu za kanisa ambazo ni Noeli, Njia ya Msalaba, Mateso ya Bwana, Pasaka na Jumatatu ya Pasaka na mikesha yote hufanyika Parokiani.
      1. 4. Vigangoni Njia za Msalaba, Misa za Sikukuu za (Noeli, Pasaka) pia hufanyika.
      1. 5. Ibada ya Kitubio kila wiki Parokiani Buyuni na wakati mwingine wa vipindi maalumu kwenye
      1. 6. Ibada za Misa Takatifu, Mazishi na ndoa Parokiani
      1. 7. Ibada za Misa Takatifu za somo kwa ajili ya VMJ…UWAKA, VIWAWA, WAWATA, MOYO MT, REJIO N.K
      1. 8. Matendo ya Upendo na Kuwajali wenye mahitaji mbalimbali ya kimwili na kiroho pasipo kuzingatia Imani yao kupitia mpango wa CARITAS wa Parokia.
      1. 9. Semina za Uongozi, Maisha ya Kiroho na Uwajibikaji kwa Kanisa Pamoja na kushiriki Hija za Kijimbo, Dekania na hija za Kiparokia kwa kalenda ya Kanisa.
      1. 10. Ibada za Misa Takatifu (Maadhimisho ya somo – Kanda na Jumuia)
      1. 11. Shughuli za Mafundisho ya Dini (Ekaristi (Jumanne, Jumatano), Kipaimara – Jumamosi kwa wote na wakatekumeni pia.
      1. 12. Huduma za mafundisho ya dini mashuleni, jumla ya walimu 6 wanafundisha katika shule za msingi 3 na secondary 3 (Buyuni, Nyeburu na Golden).
Scroll to Top